Oct 15, 2013

4 GB RAM Ubuntu Edge. Simu ya kwanza kutumia Android na Ubuntu OS kwa pamoja.


Januari mwaka huu Canonical waliitangaza Ubuntu Phone OS kama operating system mpya kwa ajili ya simu, na
sasa wanakuletea Ubuntu Edge.
Ubuntu Phone OS ni operating system ambayo inamuwezesha
mtumiaji kupata experience ya Ubuntu kwenye
simu yake kama ilivyo Windows Phone OS iliyopo kwenye Nokia Lumia.

Canonical, kampuni inayohusika na utengenezaji wa Ubuntu wameenda mbali zaidi kiteknolojia kwa kutangaza
Ubuntu Edge, ambayo itakuwa simu ya kwanza kuweza dual-boot operating system mbili kwa pamoja ambazo ni Android na Ubuntu Phone OS

                                        

Android tayari inajulikana, Ubuntu Phone OS ni operating system ambayo inampa mtumiaji uwezo wa kutumia
simu yake kama Kompyuta halisi.

                             

 Hii itawezekana pale ambapo mtumiaji ata connect simu yake na external
screen kama TV kupitia HDMI na atapata Ubuntu Desktop, kwa upande mwingine mtumiaji atatumia Ubuntu
Mobile kwa matumizi yake ya kawaida ya simu au Android.
Features
Kutokana na kuwa na uwezo wa kutumika kama kompyuta Ubuntu Edge inatarajiwa kuwa na features zifuatazo.
kioo chenye inchi 4.5 urefu hanamu 1,280 x 720 HD
si chini ya 4GB RAM
128GB memory
processor yenye uwezo mkubwa zaidi kuliko zote kipindi itakapotengenezwa (sanasana 8 core)
kioo cha sapphire crystal (utahitaji kitu kigumu kama almasi kuweka michubuko)
dual-LTE chip dual-band 802.11n Wi-Fi, Bluetooth 4, NFC
Betri ya silicon-anode Li- Ion
dual-band 802.11n Wi-Fi, Bluetooth 4, NFC
8mp low-light kamera, 2mp kamera ya mbele
GPS, accelerometer, gyro, proximity sensor, compass, barometer
micro sim
body frame ya chuma
Upatikanaji
Ubuntu Edge ni toleo maalum kwa watu ambao wangependa kuwa nayo au wapenzi wa teknolojia, hivyo
itapatikana kwa wachangiaji wa kampeni ya Ubuntu Edge kupitia Indiegogo

source: bongo electronics

No comments:

Post a Comment