Sep 22, 2013

Windows phones , Android phones..Niende wapi?

Ni kawaida sasa hivi kwenye redio kusikia matangazo ya lumia, samsung galaxies zinazidi kushika kasi, techno wanakomba soko la tanzania na huawei nyingi za tigo zinazidi kusambaa. Yote haya oyanaweza kukuchanganya na kufanya usifanye uamuzi sahihi wakati

wa kuchagua simu. Hebu tuangalie Windows Phone ni nini na Android ni nini na baadae utajua ufanyeje kuchagua simu sahihi.

Windows Phone 8
Hii ni Operating System iliyotengenezwa na microsoft inatumika kwenye simu za nokia, htc, samsung na huawei mpaka sasa. imekuja kumreplace windows phone 7 ambayo haikupokelewa vizuri na wateja. Tofauti na Android, Windows Phone inatumia tiles badala ya icon design yake hii imeipa umaarufu sana.

 Android
Hii ni Operating System iliyotengenezwa na google na inatumika na watengeneza simu zaidi ya 80 wachache wao ni samsung, htc, huawei, tecno, sony, lg na asus. Hii inatumia icon tofauti na windows phone. Pia ina homescreen ambayo unaweza kuweka app zako unazozipenda.

Je ukitaka kununua simu ya windows phone uangalie nini?

Kitu kimoja kizuri kuhusu windows phone ni uwezo wake wa kukusanya watu wote unaowajua na kuwaweka pamoja na kukupa habari zao zote. Kuna peoples hub ambayo inakua na list ya marafiki zako na kama wana acount za facebook, twitter, unaona habari zote kwenye contact bila hata kufungua app ya twitter au facebook.

Ukitoa peoples hub kuna features kama kids corner ambayo ni simu ya mtoto ndani ya simu yako, hapa unachagua application, video, miziki ambayo unataka mtoto wako aone akishika simu ili kumzua asifanye vitu vibaya. pia kuna rooms ambayo inakua ni private area kati yako na watu unaowapenda kama mke wako na wakwe zako eneo ambalo mtashare location na kila kitu. haya na mambo mengi yanaifanya windows phone kua very strong kwenye upande wa watu.

Kitu kizuri kuhusu android ina application nyingi sana. so far kuna application zaidi ya 700,000 wakati windows phone ina application 150,000 tu. hili linafanya vichwa vikubwa kama instagram kupatikana android na kukosekana kwenye windows phone.

Kwahiyo, wakati unachagua simu uangalie mahitaji yako kati ya hivyo vitu viwili hapo juu.

Microsoft vs Google
Kuna msemo siku hizi kuwa hununui simu bali unanunua ecosystem. huu msemo ni sahihi kabisa kwani kila platform siku hizi ina apps zake ambazo ni exclusive kwao tu, hapa nitaelezea ecosystem inayopatikana kwenye android na windows phone. Kupunguza ukubwa wa thread nitazi-mention tu kama utataka maelezo zaidi utacoment

• Microsoft office(wp) vs Quickoffice(Android)
• Search (bing search) vs Search (Google search)
• Map (nokia,bing map) vs Map (Google map)
• Video (hakuna) vs Video (Youtube)
• Mail (outlook,hotmail) vs Mail(Gmail)
• Cloud(skydrive) vs Cloud (Google drive)
• Video chat(skype) vs Video chat (Hangout)
•Gaming (xbox) vs Gaming (hakuna)

Hizi ni chache za muhimu so utaangalia ecosystem ipi unaipenda hapa nimeexclude apps za nokia maana ni special case.

design vs customization
Kama nilivyoelezea hapo juu Windows Phone imekuja na design mpya kabisa ya tiles ambazo ni live zinakupa information papo kwa hapo hizi tiles huwezi kuzichange na kuweka customization kama android lakini unaweza eka design unayotaka. unaweza resize tiles zikawa kubwa, za kati au ndogo na pia unaweza ukachange skin

Andoid yenyewe ipo vizuri kwenye customization kuliko windows phone unaweza ukaiweka home screen yako the way unavyopenda wewe. Zipo launcher mbali mbali zenye themes tofauti tofauti kwa kazi hii. Kwenye android pia kuna launcher ambazo zinakuwezesha kuweka themes za 3d ili kuwezesha wewe kufeel tofauti ukitumia simu

 Security vs Freedom
Kwenye Windows Phone mpaka sasa huwezi kuroot simu wala kufanya hacking ya aina yoyote simu imefungwa kila kona hili linaongeza ulinzi kwenye simu yako hutaathiriwa na virusi wala malware wa aina yoyote device itakua salama lakini tatizo linakuja unakosa uhuru hutaweza kufanya vitu unavyotaka wewe.
Kwenye Android unakua huru unaroot simu unaweka custom firmware unafanya vitu unavyotaka wewe lakini tatizo linakuja kwenye security: Android kuna malwares wengi wanaweza wasiwe virusi lakini vitu kama spyware na adware ni vigumu kuviepuka kwenye Android.

Productivity vs Playing
Nafkiri hapa ndo pa muhimu zaidi panapo zitenganisha hizi simu. Kuwepo kwa microsoft office, skydrive, photobeamer, security kubwa, offline navigation na simu kuwa fasta kunaifanya Windows Phone kuwa nzuri kwa wafanya biashara kuliko Android.
Kuwepo kwa HD games, na application mbali mbali kunaifanya android iwe simu nzuri ya kuchezea so hapa unatakiwa uangalie unahitaji nini je wewe unapenda kuchezea simu au unataka simu yako iwe productive? Maana unaweza ukaenda Windows Phone then ukakuta games chache ukaanza kulalamika;  na unaweza kuwa mfanya biashara ukaenda Android ukaanza kulalamika betry na simu kuwa slow.

Kwa hiyo haya ndio mawazo yangu kuhusu Windows Phone na Android nikiwa kama mtumiaji ambaye nishatumia platform zote. pia kuhusu windows phone nimeongelea windows phone 8 na sio 7 better unaponunua simu ya windows phone ununue 8, kama huna uhakika ni vizuri uulize.