Sep 22, 2013

Smart Accesories zazidi kuitawala dunia.

Tunaishi kwenye dunia ambayo imetawaliwa na vifaaa vya kisasa vya kieletroniki. Kwa sasa hivi dunia nzima imetikiswa na kusambaa kwa simu za mikononi zinazoitwa 'smart phones'.
Smartphones ni aina za simu za mikononi zilizounganishwa
na mfumo wa uendeshaji wa simu ukiwa umeongezewa na 
uwezo zaidi kama wa kiutendaji wa kompyuta. Simu hizi sasa zimewekewa uwezo wa kuchezesha miziki, video, kupiga picha, GPS, vioo vyake vinafanya kazi kwa kugusa tu, vivinjari wavuti kwa ajili ya kuingia kwenye tovuti mbalimbali, lakini pia zimewekewa uwezo wa kuingia/kupata muunganisho wa wavuti kwa kutumia teknolojia ya wi-fi pamoja na hizi za mobile broadband.
                               

 Wataalamu wa simu za mikononi wanasema neno smartphone halikuanza leo. Simu za kwanza kabisa kuitwa smartphone zilikuwa ni simu Eriksoni GS 88 zilizotolewa mwaka 1997 na kupewa jina kuwa ni smartphones. Kiukweli hakuna tafsiri halisi inayotambulika ya kutofautisha kati ya smartphones na simu za kawaida. Lakini kuna vitu ambavyo vinaonekana dhahiri vinavyotofautisha aina hizi mbili za simu. Moja ya tofauti kubwa kati ya smartphones na simu za kawaida ni kitu kimoja kinaitwa Application Programming Interface - API. Tofauti hii inaonyesha kuwa API kwenye smartphones inaunganisha 'mtu wa tatu' kuweza kuendesha programu zake kwenye simu hizo. Kwamba mtu huyo wa tatu anaweza kuendesha programu zikawasiliana na mfumo endeshaji wa simu hiyo au programu mbali mbali kwenye hiyo simu. Hii ni tofauti kubwa inayosemwa na watalaamu wa smartphones.
Kwa sasa hivi sio tu simu za mikononi, kumekuwa na vitu vinaitwa tablets ambazo huwezi ukaziweka kwenye fungu au kundi la simu au laptop. Zimekaa katikati.
Kampuni ya Samsung nayo imejiingiza kwa kasi kwenye teknolojia na kutoa kamera zake zenye uwezo wa 'smart'. Wameziita kamera hizi kuwa ni 'Smart Cameras'. Kamera hizi zinauwezo mkubwa wa kupiga picha na picha hiyo ukaweza 'kuitupia'   kwenye mitandao ya kijamii kama twitter, facebook n.k. Uwezo wa kamera hizi kuingia kwenye mtandao unatumia teknolojia ya wi-fi.
Teknolojia ya wi-fi kuunganisha kwenye Intaneti sio teknolojia iliyozoeleka sana kwetu Tanzania kama ilivyo kwa wenzetu nchi zilizoendelea. Simu aina ya Iphone, Samsung ambazo zilikuwa na uwezo wa kuunganisha Intaneti kwa kutumia teknolojia ya wi-fi hazikupata mafanikio Tanzania hata kidogo (Nadhani hata nchi zingine zinazoendelea ambazo teknolojia hii ya kuunganisha intaneti sio 'common'). Lakini Iphone, Ipad na Simu za samsung na samsung tablets walipobadilisha mtindo na kuongeza uwezo wa kupachika kadi za simu ili kuweza kuunganisha Intaneti sasa simu hizi na tablet hizi zimepata soko kubwa sana Tanzania. Natamani nione Kamera hizi za Samsung na zingine kama zipo ziwekewe uwezo huu wa kupachika kadi za simu ili kuziunganisha na Intaneti. Wakifanya hivi naamini Kamera hizi zitapata wateja wengi sana Tanzania na nchi zinazofanana na Tanzania.


                                                       
                                                                      Smart Camera za Samsung zenye wi-fi

 Nadhani hatutakomea kwenye simu na kamera tu. Kwa kadri teknolojia inavyozidi kuchanja mbuga sasa hivi tutaona smart printers, smart PCs na kadhalika kwa sababu Dunia imekuwa ya 'Smart Accessories'!