Oct 14, 2013

Simu 10 zenye gharama kubwa zaidi duniani.

Hii ndiyo orodha ya simu ambazo zimetambulika kuwa ndizo za 
gharama zaidi duniani kutokana na miundo yake pamoja na 
material yaliyotumika kuzitengeneza na inasemekana kuwa simu hizi zinapatikana kwa oda maalum yaani (special order). Hebu tuziangalie.



1. iPhone 5 Black Diamond - Imebuniwa na mwingereza
Stuary Hughes, na thamani yake imekuwa ya juu zaidi kutokana na logo pamoja na home button yake kuwa ni madini ya Almasi
na cava lake ni dhahabu, na hii inapatikana kwa kiasi cha dola milioni 15.3, zaidi ya shilingi bilioni 24 za kitanzania. 




2. iPhone 4 Diamond Rose Edition - Hii imetengenezwa kwa madini ya dhahabu na almasi pia katika nakshi zake zote, na bei yake ni dola milioni 8, zaidi ya shilingi bilioni 12 za
 kitanzania.
                                    

3. iPhone 3GS Supreme Goldstriker - Hii ni ya tatu katika orodha ya simu za gharama zaidi duniani, Imebuniwa na kampuni ya Goldstiker International, Imetengenezwa na kunakshiwa pia kwa madini ya almasi na dhahabu. Thamani yake ni dola milioni 3.2, zaidi ya shilingi bilioni 5 za kitanzania.
                                                               4. iPhone 3G Kings Button - Simu hii imebuniwa na mbunifu mahiri, Peter Aliosson, Imepambwa na dhahabu nyeupe na njano, Bei yake ni dola milioni 2.4, zaidi ya shilingi bilioni 3 za kitanzania. 
                                  

5. GoldVish Le Million - Hii imebuniwa na raia wa Sweeden, Emmanuel Gueit na imepambwa kwa madini ya dhahabu, special order na inamilikiwa na mfanyabiashara maarufu wa Russia, Bei yake ni dola milioni 1.3, zaidi ya shilingi bilioni 2 za kitanzania. 



                                   

 6. Diamond Crypto Smart Phone-Mbunifu wake anaitwa Peter Aloisson, Simu hii imewekewa cover ya Gold na Almasi nyingi nimetumika katika kuipatia muonekano wa    
kuvutia,Bei yake ni dola milioni 1     

                          . 
7. Gresso Luxor Las Vegas Jackpot - Hii inatajwa kama moja ya simu kali kabisa za kifahari duniani, imebuniwa na kampuni maarufu ya kutengeneza simu za kifahari ya Gresso, Dhahabu, Almasi pamoja na aina ya mbao kutoka Afrika yenye umri wa miaka 200 vimetumika katika kuunda simu hii, Bei yake ni dola milioni 1, zaidi ya shilingi milioni 161 
za kitanzania
.                                     
8. Vertu Signature Cobra - Hii imebuniwa na Vetru, ni simu ya kifahari kwa madini yaliyotumika kufanya muundo wake ila kimsingi ndani yake ina vile vitu muhimu tu na vya kawaida katika oparesheni ya simu ya mkononi, Bei yake ni dola laki 3 na 10, zaidi ya milioni 501 za kitanzania
                                   
9. Sony Ericsson Black Diamond - Simu hii imebuniwa na Garen Joh. black diamond ndiyo madinili yaliyotumika kutengeneza kava lake, ina muonekano ya kifahari na wa kiwango cha juu, Inauzwa dola 300,000. Zaidi ya shilingi milioni 484 za kitanzania.                                                                          
10. iPhone Princess Plus - Almasi imetumika kupamba muonekano na muundo wake, na bei yake ni dola 176,400, zaidi ya shilingi milioni 285 za kitanzania.

Chanzo: fm graphics