Sep 22, 2013

Gari isiyoonekana (invisible car) kutengenezwa.

Ni kitu kisicho cha kawaida ila kampuni ya magari,Benz kwa kushirikiana na wanaSayansi kutoka chuo Kikuyu cha Tokyo, wapo katika mchakato wa kutengeneza gari isiyoonekana(invisible car).Kwa mujibu wa chanzo cha habari,gari hii siyo kwamba haionekani kweli lakini
ni teknologia iitwayo 'Optical Camourflage' ndio imetumika kufanikisha hili zoezi ambalo hufanya gari lisionekane kabisa.
                                      
                                 
Teknologia hii hutumia kanuni isemayo 'ili kufanya chombo kisionekane ni lazima uone kitu kilichopo nyuma yake'.Hivyo upande mmoja wa gari huwekwa taa za LED na upande mwingine huwekwa SLR digital Cameras ambazo huchukua video za upande huo na kuoneshwa kwenye LED upande mwingine papo kwa papo.Hivyo gari inapotembea watu hawataiona gari badala yake watauona upande wa pili wa gari kupitia video, hivyo gari haitaonekana kabisa
                               
Hapa WanaSayansi wakifunga LED kwenye gari.

Licha ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, Lakini kazi imekua ngumu katika kuyafanya matairi yote yasionekane
Vilevile teknologia hii inatumika kutengeneza mnara usioonekana huko Korea ya kusini uitwao 'Seoul's Tower Infinity'.

                                    
Mnara huu kama usioonekana.