Sep 22, 2013

Kampuni ya TTCL yazindua Smartphone ili kuendana na soko.

Kampuni ya simu ya TTCL imeibuka na simu yao ya kisasa (Smartphone) ili kukimbizana na soko la simu za mikononi. Si mara ya kwanza kampuni hii inayokula pesa nyingine kutoka kwa walala hoi watanzania kwani walishawahi kuibuka na simu za mikononi

lakini zilifanya vibaya sana kwenye soko..
Kama simu hizo walizotoa zamani bado zipo basi ni chache sana humu nchini. Na kwa bahati mbaya sana kampuni hii imeshindwa kabisa kujitangaza na kulishika soko la simu za mikononi ingawa uwezo wanao kwani rasilimali zote wanazo za kuwawezesha kufanya hivyo.
Smartphone yao hiyo ni aina ya ZTE V6700 ambayo inauzwa kwa hela ya kitanzania 177,000/= pamoja na VAT.
                              


Simu hyo ina vitu hivi:
Network mode: CDMA2000
Designs: candy bar
Screen size: 3.5-inch 480x320
Screen type: capacitive screen
Camera: 3.1MP
Operating system: Android OS 2.3
RAM capacity: 256MB
ROM capacity: 512MB
Bluetooth transfer: support
GPS Navigation: Built-in GPS, support for A-GPS
Memory card: MicroSD card, support App
Keyboard Type: Virtual Keyboard
Video playback: support 3GP/MP4 format
EBook: Support